Skip to main content

Table 1 Questionnaire of the survey

From: An acceptance analysis of a sexual health education digital tool in resource-poor regions of Kenya: an UTAUT based survey study

Section A

Question English

Question Swahili

My gender is ...

Jinsia yangu ni ...

Where are you located?

Mahali uliko?

What is your year of birth?

Mwaka wa kuzali?

What is your current working status?

Hali yako ya ajira?

What is your highest educational level?

Kiwango chako cha juu cha elimu?

What is your relationship status?

Hali ya Uhusiano wako ni gani?

Do you own any of the following items?

Computer; Smartphone, Tablet, None

Je, unamiliki mojawapo ya hivi vifaa?

Tarakilishi; Simu ya rununu ya ‘Android’; Simu ya Tabuleti; La

If you want to get specific information. How often do you ...

Search online for information; Search online for health information; Search online for sexual health information

Ikiwa unataka kupata habari maalum. Ni mara ngapi wewe...

kutafuta ujumbe kwa mtandao; tafuta ujumbe wa afya mtandaoni; kutafuta ujumbe wa afya ya kujumuiana kingono mtandaoni

Please rate your digital experience.

Je, matumizi yako ya kidijitali ni mazuri kwa kiasi gani? Tafadhali pima utajriba wako wa ubunifu wa kisasa.

Section B - UTAUT

Construct

Item

Question English

Question Swahili

PU (perceived usefulness- performance expectancy)

PePu1

I find the given digital tool useful for providing sexual health information.

Naona kwamba kifaa hiki cha kidijitali ni cha muhimu kwa kusaidia kwa habari ya afya ya uzazi/kujumuiana.

PePu2

Using the given digital tool would make it easier to inform myself and others about sexual and reproductive health.

Kutumia kifaa hiki cha kidijitali kunarahisisha mimi na wengine kujipatia habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia na uzazi.

PePu3

Using the given digital tool would contribute to improvements in my sexual and reproductive health.

Kwa kutumia kifaa hiki cha kidijitali kunawezesha kuchangia kuboresha afya yangu ya kijinsia na uzazi.

PePu4

Using the given digital tool for sexual health information would enhance myself to make better and more informed decisions about my sexual and reproductive health.

Kwa kutumia kifaa hiki cha kidijitali kwa ujumbe wa afya ya ngono kunaniwezesha kufanya uamuzi kuhusu afya yangu ya kijinsia na uzazi.

EE (effort expectancy- perceived ease of use)

EePeu1

Learning to operate the digital tool for sexual health information would be easy for me.

Kujifunza jinsi ya kutumia kifaa cha kidijitali kwa kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia ni rahisi kwangu.

EePeu2

I find the digital tool is easy to use.

Napata kifaa hiki cha kidijitali ni rahisi kutumia.

EePeu3

My interaction with the digital tool to access sexual health information would be/is clear and understandable.

Kutangamana kwangu na kifaa hiki cha kidijitali ili kupata habari kuhusu afya ya kijinsia ni dhahiri na ya kueleweka vizuri.

EePeu4

It would be easy for me to become skillful at using the digital tool for sexual health information.

Ni rahisi kwangu kuwa mjuzi wa kutumia kifaa cha kidijitali cha kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia.

SI (social influence)

SI1

People who are important to me would disapprove of me using the digital tool for sexual health information.

Watu walio muhimu kwangu wanaweza kutokubaliana na mimi kutumia kifaa cha kidijitali cha kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia.

SI2

People who influence my behaviour would disapprove of me using the digital tool for sexual health information.

Watu wanao shawishi na kuathiri tabia yangu wanaweza kutokubaliana na mimi kutumia kifaa cha kidijitali kuhusu habari (ujumbe) wa afya ya kijinsia.

SI3

My family would disapprove of me using the digital tool for sexual health information.

Familia yangu inaweza kutokubaliana na mimi kutumia kifaa cha kidijitali kuhusu habari (ujumbe) wa afya ya kijinsia.

SI4

People who share the same religious belief will disapprove of me using the digital tool for sexual helath information.

Watu wenye Imani sawa na mimi wanaweza kutokubaliana na mimi kutumia kifaa cha kidijitali kuhusu habari (ujumbe) wa afya ya kijinsia.

SI5

My religious belief does not support interacting with sexual health information on a digital tool even if it is made by a credible organization.

Imani yangu ya kidini yangu hainiruhusu kutangamana na habari (ujumbe) za afya ya kijinsia kwa kifaa cha kidijitali hata kama kimetengenezwa na shirika tajika.

FC (facilitating conditions)

FC1

I have the resources necessary to use the digital tool (e.g. wifi, laptop, smartphone).

Niko na raslimali muhimu za kutumia kwa kifaa cha kidijitali (kwa mfaano[k.m] uwezo wa mtandao, tarakilishi, simu ya mkono/rununu).

FC2

I have the knowledge necessary to use the digital tool (e.g. basic digital knowledge).

Niko na maarifa ya kutumia kifaa cha digitali kama vile maarifa ya kimsingi ya kidigitali.

FC3

Using the digital tool to get sexual health information fits well with the way I like to get information.

Kutumia kifaa cha kidijitali cha kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia inaambatana na vile mimi hutaka kupata habari (ujumbe).

FC4

I think that I would use the help of a technical person to use the digital tool for sexual health information.

Nadhani naweza kuhitaji huduma za mtaalam mwenye ujuzi aweze kunisaidia kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia.

ATU (attitude towards technology use)

ATU1

Using the digital tool for sexual health information is a good idea.

Kutumia kifaa cha kidijitali ili kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia ni wazo zuri.

ATU2

Accessing sexual health information through a digital tool is more comfortable than searching other internet sources like google.

Kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinisia kupitia kifaa cha kidijitali ni bora zaidi kuliko kutumia mitandao mingine ya kutafuta habari kama google.

ATU3

I would have fun using the digital tool for sexual health information.

Naweza kuwa na furaha kwa kutumia kifaa cha digitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya ngono.

ATU4

Using the digital tool for sexual health information is interesting.

Kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia inavutia.

TA1

Using the digital tool to seek sexual health information would make me very nervous.

Kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia yaweza kunitia wasiwasi.

TA2

Using the digital tool to seek sexual health information may make me feel uncomfortable.

Kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia yaweza kunikozesha amani.

TA3

Using the digital tool for sexual health information is a bad idea.

Kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia sio wazo zuri.

TA4

Using the digital tool for sexual health information is unpleasant.

Kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia haipendezi.

BI (Behavioral Intention to use a digital tool for sexual health information)

BI2

I expect that I would use the digital tool in the future to search for sexual-health-related information.

Natarajia kutumia kifaa cha kidijitali siku zijazo kutafuta habari (ujumbe) unaoambatana na afya ya kijinsia.

BI3

I would use the digital tool for information about contraceptive products.

Naweza kutumia kifaa cha kidijitali kutafuta habari (ujumbe) kuhusu mbinu za kupanga uzazi.

BI4

I would use the digital tool for information about my menstrual period.

Naweza kutumia kifaa cha kidijitali kutafuta habari (ujumbe) kuhusu hedhi yangu.

BI5

I plan to use a digital tool to get sexual health information.

Napanga kutumia kifaa cha kidijitali kupata habari (ujumbe) kuhusu afya ya kijinsia.

Section C - SUS

Question English

Question Swahili

I think that I would like to use this system frequently.

Nadhani ningependa kutumia hii mbinu mara kwa mara.

I found the system unnecessarily complex.

Nilipata mbinu hii kuwa ngumu kiasi.

I thought the system was easy to use.

Nadhani mbinu hii ni rahisi kutumia.

I think that I would need the support of a technical person to be able to use this system.

Nadhani nitahitaji msaada wa mtaalam mwenye ujuzi ili niweze kutumia kifaa hiki.

I found the various functions in this system were well integrated.

Nilipata sehemu mbali mbali za mbinu hii zimeunganishwa vyema.

I thought there was too much inconsistency in this system.

Nafikiri kuna sehemu ambazo sio sahihi kwa mbinu hii.

I would imagine that most people would learn to use the system very quickly.

Nikidhani, watu wengi wanaweza kujifunza kutumia mbinu hii kwa wepesi.

I found the system very cumbersome to use.

Nilipata mbinu hii kuwa ya kuchosha kutumia.

I felt very confident using the system

Nalihisi kuwa na ujasiri kutumia mbinu hii.

I needed to learn a lot of things before I could get going with this system.

Nahitaji kujifunza mambo mengi zaidi kabla ya kuanza kutumia mbinu hii.